WATEULE WA MUNGU
WATEULE WA MUNGU NI WATU WA NAMNA GANI?👇
JAWABU:-
✓Ni watu ambao ni Mboni ya Jicho la Mungu mwenyewe.imeandikwa katika Warumi 8:33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
✓Wana wa Mungu na waliochaguliwa na Mungu Mwenyezi kupitia Kristo Yesu na wamejazwa nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yao.
Biblia inasema katika Yohana 15:16 "Si ninyi mlionichagua Mimi, Bali ni Mimi niliyewachagua ninyi;nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; Ili kwamba lolote mmwombalo Baba Kwa Jina langu awapeni".
✓Wamemwamini Yesu Kristo na kuokoka na Kubatizwa Kwa maji Mengi na kutengwa mbali na dhambi na wamejazwa Roho Mtakatifu.
✓Wamependwa na Mungu Na wamefanyika viumbe vipya na warithi wa Ahadi zilizo Bora hata uzima wa Milele hata Milele na Milele Amina-Yohana 3:16.
✓Watakatifu na wameoshwa mavazi yao Kwa damu ya Yesu Kristo.
✓Wamejikana na kuubeba mioyoni mwao Msalaba wa Yesu Kristo na kumfuata Mwokozi wao maisha yao yote-Marko 8:34.
✓Mwilini mwao Wamezibeba chapa(Nguvu za Roho Mtakatifu)zake Yesu Kristo-Wagalatia 6:17.
✓Wenye Haki wa Mungu alie hai na wamepewa Jina jipya na kuitwa Kwa Jina lake Mungu.👇
Tusome Isaya 43:7 MUNGU anasema hivi,
Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.
📝✍️☝️+ Ufafanuzi na mwingineo kama huo ..
Mwisho:👇
Mtu na atuhesabu hivi[Wateule wa Mungu] ,kuwa tu Watumishi wa Kristo na Mawakili wa Siri za Mungu-1Kor 4:1.
Haleluya Wateule wa Mungu,Amina na Amin.