ONLINE MISSIONARY SCHOOL
Umisionari ni utendaji unaolenga kueneza dini fulani, hasa zile zinazokusudiwa kuwa za kimataifa kutokana na misingi ya imani yake, kwamba ndivyo Mungu anavyotaka na alivyoagiza.
Asili ya neno hilo ni missio (kwa Kilatini utume).
Mmisionari au mwanamisheni ndiye mtu anayefanya kazi hiyo, hasa katika maeneo ambayo dini hiyo haipo au haijakua.
Mara nyingi wamisionari wanachangia pia maendeleo ya jamii, hasa kupitia elimu, utabibu, utunzaji wa watoto yatima na walioathiriwa na vita na maradhi mbalimbali.
Pengine uenezaji wa dini unatumia mbinu zisizokubalika kijamii, kama vile kulazimisha kwa namna moja au nyingine mtu asiyetumwa na moyo wake kukubali dini mpya.
UMISHIONARI WETU. UNATOKANA NA AGIZO LA BWANA YETU.
Mathayo 28:18-20 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁸ Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
¹⁹ Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
²⁰ na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.