SIKU 𝟙𝟘 ZA MAOMBI 𝗡𝗪𝗧𝗙🙏🏽🙏🏽
📖 NWTF – SIKU 10 ZA MAOMBI NA KUFUNGA 📖
Karibu kwenye Group la Siku 10 za Maombi na Kufunga lililoandaliwa na NWTF.
Hili ni jukwaa la waumini kuungana kwa moyo mmoja, tukijinyenyekeza mbele za Mungu kwa kufunga, kuomba, kutafakari Neno la Mungu, na kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu.
🎯 Lengo la Group:
Kuimarisha maisha ya kiroho
Kutafuta uso wa Mungu kwa unyenyekevu
Kuombea kanisa, familia, taifa na huduma ya NWTF
Kujengwa na kuhamasishana katika safari ya imani
📖 Misingi ya Group:
Neno la Mungu
Maombi na kufunga
Nidhamu, heshima na upendo
Kuepuka mijadala isiyohusiana na maombi
🙏 “Ikiwa watu wangu waliojulikana kwa jina langu watajinyenyekeza…” (2 Nyakati 7:14)
Karibu tushirikiane kwa siku 10 za kumtafuta Mungu kwa bidii, tukiamini mabadiliko, ufufuo na majibu ya maombi.
Karibu sana – Mungu yupo kazini! 🔥🙏