MIJADALA KWELI YA INJILI INTERNATIONAL MINISTRY
*SHERIA NA TARATIBU ZA GROUP MIJADALA INJILI YA KWELI INTERNATIONAL MINISTRY*
Group hili Ni group huru kwa kila mtu, kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu kwanjia ya mijadala, mafundisho na maswali n.k.
1 *NI RUHUSA KWA KILA MTUMISHI KUHUBIRI NENO LA MUNGU MDA WO WOTE, KATIKA HAKI NA KWELI YA INJILI YA KRISTO BILA KUPANGWA KWENYE RATIBA.*
Wakolosai 3
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
__________________________
2 *TUNARUHUSU MADA KUJADILIWA MOJA MOJA, KWA UTARATIBU MOJA BAHADA NYINGINE KWA FAIDA YA KILA MTU.*
1 Petro 3
15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
_________________________
3 *MADA IKIWA NGUMU NI RUHUSA KUINGIA CONFERENCE ,KWA MAELEZO ZAIDI*
__________________________
4 *INARUHUSIWA KWA KILA MTU KUTOA MADA , ILA ZAMU KWA ZAMU* .
__________________________
5 *MSAHADA KWA MMOJA WETU MWENYE SHIDA, MSIBA, HARUSI N.K INARUHUSIWA KAMCHANGIA NDUGU KATIKA KRISTO, SI KWA LAZIMA WALA KWA SHERIA,BALI KWA HIARI* Wagalatia 6
10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
__________________________
6 *MATUSI NA DHARAU HAVIRUHUSUWE. UKI ONYWA MARA 3 KAMA HUSIKIE, BASI UTA TOLEWA KWENYE GROUP.*
Waefeso 5
3 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
4 wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.
__________________________
7 *WATUMISHI WANAO*
*FUNDISHA MARUFUKU KUOMBA* *PESA AU* *SADAKA KWA KUKAZA NA* *KULAZIMISHA WATU,* *HUSIKIE* *UTATOLEWA NJEE*
2 Wakorintho 9
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
__________________________
8 *HAIRUHUSIWE KUTONGOZA WAKE ZA WATU AU KUSUMBUA WATU INBOX, HUSIKIE UTATOLEWA
By Ev Mayenge Dieumerci S