SALA-NOVENA-MAOMBI
🌿✨🙏 UONGOZI WA SALA, NOVENA, MAOMBI NA SADAKA 🙏✨🌿
UTANGULIZI:
Kundi hili limeanzishwa kwa ajili ya kuwaleta pamoja waamini kama familia moja ya Kikristo. Ni mahali pa sala, mshikamano, upendo na kujengeana imani. Tunakusanyika kwa pamoja ili kumtukuza Mungu, kuombeana, kushirikiana katika Novena, na kuunga mkono kazi za Mungu kupitia sadaka za hiari.
DIRA:
Kujenga jumuiya ya Kikristo yenye mshikamano wa kiroho na kijamii, inayosali kwa bidii, kushirikiana kwa sadaka na kuishi ushuhuda wa imani hai.
DHIMA:
Kuwaleta pamoja Wakristo kwa ajili ya sala, Novena, maombi na sadaka za hiari; kukuza mshikamano, kushirikiana katika changamoto za maisha, na kushuhudia upendo wa Mungu kwa maneno na matendo.
MALENGO MAKUU:
1. Kuwaunganisha wanakikundi kupitia sala na Novena za kila siku.
2. Kuimarisha mshikamano wa Kikristo kwa kushirikiana kiroho na kimwili.
3. Kukuza mshirikiano na moyo wa kusaidiana kupitia sadaka za hiari.
4. Kuombea familia, Kanisa, taifa na mahitaji binafsi ya kila mwanakikundi.
5. Kufundishana mafundisho ya imani ili kukuza maisha ya kiroho.
THAMANI KUU:
🌟 Imani thabiti kwa Mungu
🌟 Upendo wa kweli kwa Mungu na jirani
🌟 Mshikamano na mshirikiano wa dhati
🌟 Ukarimu na moyo wa kutoa sadaka za hiari
🌟 Unyenyekevu, nidhamu na heshima
🌟 Kuwa mashuhuda wa amani na imani hai
KANUNI ZA KUNDI:
✅ Kudumisha heshima na mshikamano kati ya washiriki wote.
✅ Kushiriki kikamilifu katika sala, Novena na sadaka (kwa hiari).
✅ Kuweka kundi kwa ajili ya mambo ya kiimani pekee.
✅ Kuombeana, kusaidiana na kushirikiana katika changamoto na baraka za maisha.
📖 “Kila mmoja na atoe kadiri alivyoazimia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa kulazimishwa; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa furaha.” (2 Wakorintho 9:7)