MAKALA ZA MWL. MAKUNGU
*UTARATIBU WA KUNDI LETU*
Mjumuiko wetu humu ndani ni wa watu wenye mapenzi na chachu ya kupata maarifa ya mambo mbalimbali ya kisaikolojia,kifalsafa,kiimani, kisiasa na kijamii huku tukihusianisha na maandiko matakatifu kupitia makala zinazotafakarisha na kujenga jamii yenye uelewa mpana wa mambo zaidi ya vile walivyokuwa wanayaelewa..
Yoyote Kati yetu anaruhusiwa kushare pamoja nasi makala nzuri ya kutujenga kifikra na kuponya utu wetu . Iwe ni makala ya kutafakarisha na kujenga.
Ukurasa wetu huu siyo ukurasa wa kuchati au kubishana kwa hoja ngumu kiushindani . Bali ni sehemu ya kusoma maarifa ya fikra tunduizi na kuelewa kwa utulivu Kama library.
Unaweza kupongeza , kuongezea kitu ,kujadili pale panapohitajika ,ama kufafanua jambo . Ili kujengana zaidi .
Mjumuiko wetu humu ni wa watu wa kada mbalimbali na umri tofauti tofauti. Hivyo ni muhimu kuzingatia heshima na maadili.
Tuna viongozi wa dini, viongozi wa serikali , viongozi wa vyama vya siasa, watumishi, wahadhili wa vyuo vikuu, wafanyabiashara,wakulima na wasomi mbalimbali.. group namba mbili