ELIMU YA UJENZI NA RAMANI BORA
Karibu sana wadau wote!
Group hili limeanzishwa kwa ajili ya kupeana uzoefu kuhusu ujenzi wa nyumba zako na za wateja wako.
Hapa utapata:
• Mafundi waaminifu wa kazi zote
• Bidhaa bora za ujenzi
• Ushauri na majibu ya maswali yote yahusuyo ujenzi
• Fursa za viwanja, mashamba, nyumba zinazouzwa na za kupangisha
• Ramani mbalimbali za nyumba na ushauri wake
Unaruhusiwa:
• Kushirikiana na kushauriana mawazo kuhusu ujenzi wa nyumba
• Kujadili mada zinazohusu ujenzi
• Kutangaza biashara inayohusiana na sekta ya ujenzi (Ijumaa na Jumapili pekee)
• Kutangaza viwanja vinavyouzwa, mashamba yanayouzwa, nyumba zinazouzwa, nyumba za kupangisha na ramani
Hairuhusiwi:
• Lugha za matusi au kejeli
• Picha au maudhui yasiyo na maadili
• Mijadala isiyohusiana na ujenzi
• Kutuma matangazo mara kwa mara bila mpangilio (spam)
• Kutuma namba binafsi za watu bila idhini
Ukikiuka masharti haya, utaondolewa kwenye group bila taarifa na hautarejeshwa tena.
Karibu tujenge pamoja!
Nyumba bora hujengwa na fundi bora