MOYO WA MWAMINI (the heart of Believers)
📜 KANUNI ZA MOYO WA MWAMINI
1. Lazima Uwe umeokoka na Kristo awe kiini cha yote
Uwe tayari kuishi maisha matakatifu ya kumtukuza Yesu Kristo.
📖 Wakolosai 3:17
2. Neno la Mungu liwe msingi
Tunashiriki mafundisho yenye kuzingatia Biblia, si nadharia za watu.
📖 2 Timotheo 3:16
3. Uwe umejaa Roho Mtakatifu aheshimiwe. Na unaushuhuda wa kujzwa
📖 Yohana 16:13
4.Upendo na heshima kwa wote
Hakuna matusi, kejeli, mahusiano ya kijinga, ugomvi au maneno ya kushambulia.
📖 1 Wakorintho 13:4–7
5. Epuka mabishano yasiyo na tija
Masuala ya siasa, udini wa kushambuliana, Matusi, mabishano yasiyojenga hayaruhusiwi.
📖 Tito 3:9
6.Tunajenga, Tunabomoa mafundisho Potofu.
Nje ya Muktadha wa biblia.
📖 Waefeso 4:29
7.Maombi na ushuhuda vinakaribishwa
Ushuhuda uwe wa kweli na wa kumtukuza Mungu, si kujitukuza mtu.
📖 Zaburi 66:16
8.Nidhamu ya Kikristo iheshimiwe
Anayekiuka kanuni atakumbushwa kwa upendo; akiendelea, atachukuliwa hatua stahiki. (Ukikiuka kanuni mojawapo utachukuliwa hatua pamoja na kutolewa)
📖 Mathayo 18:15–17
9.Hakuna matangazo ya biashara bila ruhusa
Group ni kwa ajili ya huduma, si soko.
Tunakuwa watendaji wa Neno
Lengo letu si kusikia tu, bali kuishi Neno la Mungu.
📖 Yakobo 1:22