NURU YA UJIO WA PILI WA YESU KRISTO,
📖 SHERIA ZA GROUP LETU NI📖
1.Heshima ni lazima
Kila mwanachama ataheshimu wengine bila matusi, kejeli au lugha chafu.
2.Lengo la group liheshimiwe
Group ni kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu, maombi na kujengana kiroho. Mambo yasiyoendana na kusudi hili hayaruhusiwi.
3.Epuka maudhui yasiyofaa
Hairuhusiwi kutuma picha, video au ujumbe usio na maadili au usio wa kiroho.
4.Hakuna matangazo bila ruhusa
Biashara, matangazo au promosheni yoyote itaruhusiwa tu kwa idhini ya viongozi wa group.
5.Hakuna siasa wala mijadala ya kugombana
Mijadala ya kisiasa au inayoweza kuleta mgawanyiko hairuhusiwi.
6.Weka nidhamu ya kutuma ujumbe
Epuka kutuma ujumbe mwingi usio na maana (spam), au ujumbe nje ya mada.
7.Heshimu muda wa group
Kama kuna ratiba ya maombi au mafundisho, izingatiwe.
8.Usiri wa group ulindwe
Yaliyojadiliwa ndani ya group yabaki ndani ya group isipokuwa kwa ruhusa.
9.Kukosoa kwa upendo
Marekebisho yafanyike kwa upendo na heshima, si kwa hasira.
10.Adhabu kwa uvunjaji wa sheria
*.Onyo la kwanza
*.Onyo la pili
*.Kuondolewa kwenye group